Kuelewa trade ya siku moja ya crypto: mikakati, vidokezo na makosa ya kuepuka

Stanislav Bernukhov

Mtaalamu Mkuu wa Kutrade wa Exness

Anza kutrade

Huu sio ushauri wa uwekezaji. Utendaji wa awali sio dalili ya matokeo yajayo. Mtaji wako uko hatarini, tafadhali fanya biashara kwa uangalifu.

Shiriki

Ikiwa wewe ni trader aliye na uzoefu au anayeanza wa crypto, mwongozo huu utakufaa. Katika mwongozo huu, tunaangazia baadhi ya mitindo na mikakati ya biashara ambayo iko chini ya kategoria ya trade ya siku moja, tukimakinika zaidi kwenye cryptocurrencies. Pia tutaangazia baadhi ya faida na changamoto za trade ya siku moja ya crypto.

Je, trade ya siku moja ni nini?

Kabla ya kuangazia mada hii kwa kina, hebu tufafanue maana yake. Je, trade ya siku moja ni nini? Trade ya siku moja ni hali ya kununua na kuuza amana, kama vile stocks, jozi za sarafu, bidhaa, au cryptocurrencies, ndani ya siku moja ya biashara, ili kuepuka kukabiliwa na hatari za soko za usiku kucha.

Mtindo wa trade ya siku moja kwa crypto 1: Scalping

Mtindo wa trade ya siku moja unaosonga haraka zaidi ni scalping, na unalenga kupata faida kutokana na mienendo midogo ya bei.

Scalping ilianza katika maeneo ya awali ya biashara ambapo traders walikuwa wanakutana kufanya biashara ya instruments za kifedha na biashara ilifanywa ‘kwa njia ya mdomo.’ Traders katika maeneo haya walikuwa scalpers, walikaa katika upande tofauti na brokers, ambao walitekeleza positions za wateja wao. Ndiyo maana scalpers waliitwa pia ‘market makers.’

Siku hizi, scalper ni trader wa kawaida kwenye skrini ambaye hutumia leverage ya juu na hufanya trades za haraka, akijaribu kunufaika kutokana na mienendo midogo ya bei au mabadiliko ya bei karibu na support au resistance level. Kwa kawaida, scalper hushikilia trades kati ya sekunde na dakika kadhaa.

Cryptocurrencies zinajulikana kwa volatility inayobadilika ikilinganishwa na aina zingine za mali. Lakini, sio kila wakati: kwa mfano, katika majira ya joto ya 2023, volatility ya Bitcoin ilikuwa katika kiwango cha chini zaidi, na hakukuwa na mienendo mikubwa katika soko. Hapa ndipo scalping inapoweza kutumika: inaweza kuruhusu trader kufanya biashara hata katika soko lenye volatility ya chini, kwa kuwa scalpers hawatafuti faida kubwa na wanaweza kupata faida ndogo ya pips kadhaa.

Mfano wa mabadiliko madogo ya bei ambayo traders wa siku moja na scalpers wanaweza kunufaika nayo.

Faida na hasara za scalping katika crypto

Faida za scalping

  • Scalping inaweza kuwa njia ya haraka zaidi ya kukuza akaunti ikifanywa kwa njia inayofaa.
  • Kwa kuwa kiwango cha biashara cha scalpers kiko juu ikilinganishwa na traders wa aina zingine, wanafanya trades zaidi, na kuna uwezekano wa, faida zaidi.
  • Scalpers hawakabiliwi na hatari ya usiku kucha: muhimu sanasana kwa crypto, ambayo bei yake inaweza kushuka ghafla wakati wa usiku.
  • Scalpers hufanya kazi tu wakiwa kwenye skrini, kwa hivyo hawahitaji kushikilia positions na kuathiriwa na volatility ya ghafla.

Hasara za scalping

  • Inahitaji umakini wa kiwango cha juu;
  • Inaleta gharama kubwa za biashara kuliko za kawaida (kama spreads). Masoko ya Crypto yanaweza kuleta gharama kubwa zaidi kuliko za kawaida, kwa kuwa volatility inayotarajiwa ya cryptocurrencies iko juu ikilinganishwa na masoko ya sarafu zinazotolewa na serikali. Ndio maana market makers katika crypto kwa kawaida huweka spreads kubwa kwa BTC, ETH, na mali sawa.
  • Scalper wa kawaida anahitaji kufikia kiwango cha juu cha trades ili kuendelea kupata faida;
  • Scalper huathiriwa zaidi na makosa kuliko trader mwingine yeyote: kwa vile uwezo wa kupata faida wa scalper ni mdogo, idadi ya trades zenye mafanikio inahitaji kuwa ya juu kila wakati kwa scalper.

Scalping ni mtindo ambao kwa kawaida unapendekezwa kwa traders wenye uzoefu kwa kuwa unajumuisha kiwango cha juu cha biashara na gharama kubwa - na unahitaji uangalizi wa karibu wa mienendo ya bei wakati trades zimefunguliwa. Iwe unafanya trade ya cryptos au madaraja mengine yoyote ya mali katika Exness, tunapendekeza ujaribu kwanza, kwenye akaunti ya demo au Akaunti ya Standard Cent.

Mtindo wa pili wa trade ya siku moja ya crypto: Trade ya siku moja inayoendelea

Trade inayoendelea ya siku moja, kwa ujumla, ni mtindo wa biashara usiokuwa na mienendo mingi kama scalping na kwa kawaida unamaanisha kuanzia trade moja ya siku moja hadi idadi ndogo ya trades kwa kila siku.

Unaweza kutumia mtindo huu wa biashara wakati wa kupanda kwa bei ya BTCUSD, ETHUSD au mali nyingine za crypto, kwa kuwa zinaweza kutoa breakouts kubwa na kutoa uwiano mzuri wa faida/hasara kwa trades zako.

Kumbuka: uwezo wa bei kuwa na mienendo mikubwa ndani ya siku moja uko chini. Siku zenye mienendo mikubwa sana ya bei hutokea kwa mara chache sana, kwa hivyo sharti trader awe mwangalifu sana akichagua trades, kwa kuwa uwezekano wa ‘mabadiliko yasiyotarajiwa’ katika hatua ya bei na bei kubaki katika kiwango kimoja unaweza kuwa juu. Bado, kunaweza kuwa na ‘siku za kipekee’ zilizo na volatility isiyo ya kawaida: hutokea wakati wa ‘kupanda kwa bei kwa kiwango kikubwa’ au ‘mali zinauzwa kwa haraka kutokana na uwoga’.

Hata hivyo muda ni muhimu kwa trader yeyote wa siku moja aliyefanikiwa wakati wa kununua na kuuza crypto. Kubashiri kwa usahihi kiwango ambacho bei itafikia hakutoshi: ni muhimu pia kufungua position hiyo ukiwa na hatari ya chini kabisa na kuweka stop loss thabiti.

Ndiyo maana, trade ya siku moja kwa kawaida inaonekana zaidi kama kazi ya mchana, sio kama burudani ya kompyuta ndogo kwenye kochi karibu na ufuo wa bahari. Bado, wewe, kama trader, unaweza kufanya biashara popote ulipo duniani, ikiwa una muunganisho wa kutegemewa wa mtandao na unaweza kumakinika kwenye masoko ya kifedha.

Mikakati ya trade ya siku moja ya kutrade crypto

Mikakati tofauti ya trade ya Siku moja ambayo traders wa siku moja katika soko la cryptocurrency hutumia hutegemea mtindo wao wa biashara. Kwa mfano, ikiwa wewe, kama trader wa siku moja, ungependa trade moja nzuri ya siku moja kwa siku, unaweza jaribu kutafuta points za mabadiliko ndani ya siku hiyo. Hebu tuangalie aina hii ya biashara kwa kina zaidi.

Mkakati wa kwanza wa trade ya siku moja: kupata points za mabadiliko

Points za mabadiliko zinazowezekana zinaweza kutokea katika sehemu zenye support au resistance ya juu, kama inavyoonyeshwa katika mfano ulio hapa chini: BTCUSD ilikuwa imekaribia kiwango cha 29700, kiwango cha chini zaidi kilichokuwa kimefikiwa kuanzia tarehe 7 Julai. Baada ya kufikia kiwango hiki, shughuli ya ununuzi ilirejea kwenye soko, na kuwezesha trader wa siku moja kunufaika na kupanda kwa mwenendo wa kwa bei. Jambo la kushangaza hapa lilikuwa kwamba hatua ya bei iliyotajwa ilifanyika baadaye mchana kwa saa za Ulaya, kumaanisha kuwa ni traders wachache waliokuwa karibu na skrini zao wakati wa tukio hilo.

Mfano wa kupanda kwa mwenendo wa bei, ambao trader wa siku moja angenufaika nao kwa kufungua position ya ununuzi.

Mkakati wa pili wa trade ya siku moja: trade ya siku moja ya mwenendo wa bei ya crypto

Kufuata mwenendo wa bei ni mkakati ambao umekuwa tangu kuanzishwa kwa soko. Ingawa inaweza kuwa jambo la busara kujaribu “kununua bei ikiwa chini” na “kuuza bei ikiwa juu”, traders wa siku moja waliofanikiwa ambao wanafanya trade ya kufuata mwenendo wa bei huzingatia kununua mali ambayo bei yake “tayari iko juu” ili kuiuza bei ikiwa “juu zaidi”. Jambo la kuvutia kwa trade ya kufuata mwenendo ni kwamba inaweza kumpa trader wa siku moja faida ya haraka, kwa kuwa mwenendo unaoongezeka kwa kiwango cha juu husukuma bei haraka huku viwango vikiongezeka.

Mkakati wa tatu wa trade ya siku moja: breakouts za trade katika masoko ya crypto

Breakout ni hatua ya bei ya haraka inayosukuma bei ipite kiwango fulani au muundo fulani wa chati, au kupitia kiwango fulani cha mtindo wa trend unaoenda kinyume na trend kuu. Ufuatao ni mfano wa breakout iliyotokea katika BTCUSD mnamo Julai 2023:

Mfano: Breakout ya BTCUSD mnamo Julai 2023. Baada ya breakout ya haraka, bei ilibadilika na kufungwa chini ya bei ya kufunguliwa.

Katika mfano huu mahususi, inaonekana kuwa breakout ilikuwa ya haraka, ingawa pia iliisha haraka. Hata hivyo, kama trader wa siku moja, hii inaweza kuwa fursa nzuri kwa trade ya muda mrefu ndani ya siku moja, kwa kuwa ungeweza kuweka stop-loss ndogo na kupata faida ya haraka na ya kuridhisha ndani ya siku moja. Sio breakouts zote zinazokuwa na mwendelezo thabiti. Kwa sababu hiyo, masoko ya crypto yanahitajika kuwa ndani ya awamu ya ‘kupanda kwa bei’. Hata hivyo, kwa trader wa siku moja, mienendo midogo ndani ya siku moja bado inaweza kutoa uwiano mzuri wa faida/hasara.

Mkakati wa nne wa trade ya siku moja: trends za siku moja zinazofuata trend katika crypto

Katika trade ya siku moja inayofuata trend inayotumika kwa masoko ya crypto, tunaangazia mienendo ya bei ya haraka na isiyobadilika, inayodumu kwa siku chache tu, badala ya trends za muda mrefu au muda wa wastani ambazo zinadumu kwa wiki au hata miezi. Trends hizi za muda mrefu za kununua na kuuza amana ziko chini ya aina tofauti za mikakati, kama vile trade ya muda mfupi au ya position. Trader wa siku moja mwenye ujuzi anayeona trend kama hii ya muda mfupi anaweza kutumia mkakati wake wa biashara ya siku moja pamoja na trend hii kwa siku kadhaa mfululizo hadi itakapoisha.

Kinyume na mbinu hii, traders wa siku moja na traders wa position mara kwa mara hulenga "kununua bei ikienda chini," wakitarajia kuwa kutakuwa na mabadiliko katika mwelekeo wa trend. Traders wa siku moja, kwa upande mwingine, wanapendelea kunufaika kutokana na mwenendo wa bei pamoja na trade ya kufuata mtindo katika mkakati wao. Njia hii hutumiwa sana na traders wa siku moja waliofanikiwa kupata fursa za biashara kwa soko linalobadilika haraka la crypto.

Hebu tuangalie mfano ulio hapa chini unaohusisha BTCUSD:

Mfano: Trend ya BTCUSD mnamo Oktoba 2023. Bei ilishuka hadi moving average (50) na kumpa trader fursa ya kufungua position ya ununuzi.

Trend hiyo ilipoanza mnamo Oktoba 2023, bei hiyo ilipata breakouts kadhaa za muda mfupi, kisha ikashuka hadi kwa moving average ikiwa na kigezo cha 50 kwenye chati ya dakika 60. Hiki ni kigezo cha kielelezo tu, kinachotolewa kwa madhumuni ya uelekezi, lakini hiyo ndiyo kanuni inayoweza kutumika sio tu kwenye vipindi vidogo vya muda lakini pia kwenye chati za kila siku: bei ya trends zinazoendelea hushuka kwa muda mfupi hadi kwa kiwango kinachobadilika ambapo bei inaacha kushuka. Katika mfano huu, kiwango hiki huonyeshwa na indicator ya moving average. Trader wa siku moja katika masoko ya crypto anaweza kutumia points hizo kwa manufaa yake, na kufungua trades katika mwelekeo huo wa trend.

Bila shaka, si kila trend katika crypto inayoweza kuendelea. Lakini, ikitambuliwa kwa usahihi, trend hukupa mwelekeo wazi, na unapaswa kuzingatia muda na execution yake.

Changamoto za trade ya siku moja ya crypto

Kila mtindo wa biashara una changamoto zake, na vile vile trade ya siku moja.

Kwa upande mmoja, traders wa siku moja hujaribu kushikilia positions usiku kucha, ili kuwa na utulivu. Trade ya siku moja ya Crypto inaweza kulazimisha trader kukabiliana na volatility ya siku moja, ambayo inaweza kusababisha hasara. Ukwasi mkubwa na kupanda kwa bei kwa ghafla ni jambo la kawaida kwenye masoko ya crypto, hata kwa Bitcoin. Altcoins zinaweza kutoa volatility kubwa zaidi kuliko BTCUSD kwa pande zote za hatua ya bei.

Huenda ikawa vigumu kusubiri fursa nzuri ya biashara kwa saa kadhaa, kisha unapofungua trade, uone bei ikibadilika ghafla na kumaliza faida ya biashara ya siku nzima kwa dakika chache. Hii inaweza kutokea, kwa mfano, kutokana na matokeo ya habari za kifedha zisizotarajiwa au machapisho mengine yanayohusiana. Ingawa, wakati mwingine masoko ya crypto hayahitaji habari zozote za kifedha ili kuanzisha hatua. Mabadiliko yanaweza kuwa matokeo ya uvumi fulani kwenye mitandao ya kijamii, ambao hutokea kuhusu crypto kila wakati, na inaweza kusababisha athari sawa.

Traders wanapaswa kufahamu hisia za kuchanganyikiwa na tamaa ambayo inaweza kuwasukuma kufanya 'trades za kulipiza kisasi', na hatimaye kusababisha kufanya biashara ya kupita kiasi.

Kufanya biashara kupita kiasi katika trade ya siku moja

Kufanya biashara ya kupita kiasi kunahusisha kufanya trades nyingi zaidi ya zinazofaa. Huenda ikawa ni matokeo ya kufanya biashara kiholela kwa kufuata kihisia, au trades ambazo zinaweza kubainishwa kama za 'kimfumo', ingawa zinaweza kuwa hazifai kwa masharti ya sasa ya biashara.

Tukiunda takwimu za biashara na kulinganisha utendaji na idadi ya trades, kufanya biashara ya kupita kiasi kunamaanisha kufanya trades nyingi na kupata matokeo hasi. Ikiwa tutajumuisha kuongezeka kwa gharama za biashara zinazohusiana na crypto, kufanya biashara ya instrument hiyo kupita kiasi ni suala kubwa kwa traders wa siku moja.

Mtindo wa kufanya biashara kupita kiasi huonekana kama: kuongezeka kwa idadi ya trades kunahusishwa na kupoteza pesa kwa kiasi kikubwa, ambayo ni matokeo ya moja kwa moja ya kufanya biashara kupita kiasi. Ikiwa uko katika kategoria hii, hauko pekee yako. Traders wengi wa siku moja wanakabiliwa na suala hilo.

Chanzo: Utafiti wa kibinafsi wa utendaji wa biashara wa baadhi ya traders kupitia huduma hiyo https://en.webmarketstat.ru/

Jinsi ya kuepuka kufanya biashara kupita kiasi

Traders wengi wa kitaaluma wa siku moja katika masoko ya crypto hutumia udhibiti wa hatari unaobadilika. Kumaanisha kuwa, wanaweza kupunguza kiwango chao ikiwa wanapoteza pesa ndani ya siku fulani hadi wapate ujasiri na kuanza kufanya trades zenye faida tena. Sio tabia mahususi ya biashara kwa traders wa crypto: traders wa kitaaluma katika masoko yote hufanya hivi.

Traders fulani wa siku moja hufanya kazi ndani ya muda fulani pekee na kupunguza idadi yao ya trades. Hiyo haiwezi kutumika kwa scalpers, kwa kuwa scalper anahitaji kuendelea kutrade, lakini udhibiti unaobadilika wa hatari bila shaka utasaidia.

Hata hivyo, bila kujali mtindo wa biashara unaotumiwa, scalping au biashara ya siku moja, ni muhimu kuepuka kufungua trades nyingi, ili kuzuia uchovu.

Kanuni kuu hapa ni kuenda mapumzikoni, kupunguza ukubwa wa trade yako kwa muda, au hata kubadili kwa muda hadi akaunti ya cent au ya demo, ili kurejesha imani. Masoko bado yatakuwepo kesho, na ni muhimu kuhifadhi mtaji wako na afya yako ya kihisia. Usifanye trades nyingi za siku moja. Zingatia ubora wa trades zako, sio wingi.

Ni instruments gani za crypto za kuchagua kwa biashara ya siku moja

Jambo lingine muhimu la biashara ya siku moja katika crypto ni kuchagua instrument sahihi.

Ni nadra kwa traders wa siku moja kufanya trades zenye mafanikio kwenye masoko na skrini nyingi. Ni bora kuchagua instrument moja au mbili, na kuzingatia hizo pekee.

Bitcoin na Ether ndizo instruments bora, kwa kuwa zina volatility na liquidity ya kutosha ya soko ili kuepuka slippages na kuongezeka kwa spreads. Hiyo ni muhimu sana, kwa kuwa instruments za crypto zenye liquidity ndogo zinaweza kusababisha slippage na kuongezeka kwa spreads.

Chagua instruments zako kwa makini, na uzingatie jinsi unavyoitikia hali na uvumilivu wa hatari ili kuzuia mafadhaiko na uchovu usio wa lazima. Tazama orodha kamili ya jozi za crypto zinazopatikana zinazotolewa na Exness.

Trade ya Siku Moja ikilinganishwa na trade ya muda mrefu - ni ipi inayofaa kwako?

Kama unavyoweza kuwa unajua, hakuna mkakati au mtindo wa biashara unaokuhakikishia mafanikio. Kila trade huja na kiasi fulani cha hatari. Ndio maana kujua ni mtindo gani wa biashara unaolingana na njia yako ya maisha na malengo ni hatua ya kwanza, na kuchagua broker sahihi ni hatua ya pili.

Trade ya siku moja inahitaji kujitolea na umakini thabiti, ilhali mitindo mingi ya biashara ya muda mrefu kama vile biashara ya position na hata biashara ya muda mfupi inaweza kuendana na mtindo wa maisha wenye shughuli nyingi na muda mfupi zaidi wa kukaa kwenye skrini.

Maswali yanayoulizwa sana

Zana bora zaidi za uchanganuzi wa kiufundi kwa trade ya siku moja ni muhimu kwa traders waliofanikiwa kufanya maamuzi sahihi. Traders wa mwenendo wa bei mara nyingi hutegemea zana hizi ili kuchunguza mienendo ya bei na kubashiri bei za mali za siku zijazo ndani ya siku hiyo hiyo.

Zana kuu za uchanganuzi wa kiufundi

Indicators muhimu za kiufundi zinazotumika mara nyingi kwa trade ya siku moja ni pamoja na moving averages, relative strength index (RSI) , moving average convergence divergence (MACD), na volume indicator.

Indicators hizi za kiufundi husaidia traders kutambua points zinazowezekana za ununuzi na uuzaji, na kuwasaidia kutambua trade inayoweza kuleta faida. Kwa mfano, moving averages inaweza kusaidia kutambua masoko yanayovuma, RSI inaweza kuonyesha hali ya kununuliwa au kuuzwa kupita kiasi, na volume indicator inaweza kuonyesha kiwango cha ada au shughuli katika soko.

Ikihitajika, trader anaweza kutumia indicators hizo kwa wakati mmoja. Hapa chini kuna mfano wa trade ya ununuzi kulingana na RSI katika mwelekeo wa trend, unaotambuliwa na moving averages.

Trend ya ETHUSD mnamo Novemba 2023 ilikuwa juu, kama ilivyoonyeshwa na moving averages mbili, ingawa muda wa kuingia haukuwa sahihi. Indicator ya RSI ilisaidia kuboresha muda na kuingia kwa bei nzuri zaidi baada ya kushuka kwa bei.

Mahali zana hizi za kiufundi zinaweza kupatikana

Brokers wa mtandaoni mara nyingi hutoa zana za uchanganuzi wa kiufundi, lakini traders wanaweza pia kutumia majukwaa mengine ya kuweka chati. Traders hutumia zana hizi kubainisha points zao za kuingia na kutoka kabla ya soko kufungwa, na kuhakikisha kuwa hawashikilii positions za usiku kucha. Katika masoko ya crypto, hakuna bei za kufunga, kwa kuwa soko hili hufanya kazi kila wakati, ingawa kuna vipindi ambavyo kuna shughuli nyingi au chache za biashara.

Kwa hivyo, kuelewa na kutumia kwa usahihi zana hizi kunaweza kusababisha mikakati ya biashara ya siku yenye mafanikio.

Uchanganuzi wa kimsingi una jukumu katika trade ya siku moja, ingawa umuhimu wake unatofautiana kati ya traders wa siku moja. Traders wa siku moja hutumia brokers wa mtandaoni wanaotoa huduma za udalali kununua na kuuza crypto na financial instruments zingine siku nzima, mara nyingi hutegemea mwitikio wa soko wa muda mfupi kwa habari na matukio ili kubaini trades zao.

Tukio la utafiti na hali ya tasnia

Ingawa baadhi ya traders wa siku moja wanaweza kuangazia uchanganuzi wa kiufundi zaidi, wengine wanaweza kujumuisha utafiti wa kimsingi kwenye mikakati yao ya biashara. Aina hii ya uchanganuzi inajumuisha kutathmini uwezo wa kifedha wa kampuni, hali ya tasnia, na trends za soko, kati ya mambo mengine. Kwa mfano, traders wa siku moja wanaweza kutumia aina hii ya uchanganuzi kutathmini ripoti ya mapato, kubashiri jinsi soko litakavyoitikia.

Katika masoko ya crypto, uchanganuzi wa kimsingi sio rahisi sana, lakini wakati mwingine traders hutumia uchanganuzi wa shughuli na transactions, wakijaribu kufuatilia mienendo mikubwa za mtaji kati ya pochi na ubadilishanaji. Pia, masoko ya crypto yana uhusiano fulani na stocks, ndiyo sababu traders wa crypto wanaweza kufaidika kutokana na kujua mwelekeo wa mienendo za indices kuu za stock.

Uchanganuzi wa kimsingi unaweza kusaidia kupunguza hatari

Ni muhimu kukumbuka kuwa trade ya siku moja ni hatari. Traders wengi wa siku moja hupoteza pesa, hasa wale ambao ni wapya kwa biashara au ambao hawatekelezi mikakati ya kupunguza hatari. Kwa hivyo, kutumia utafiti wa kimsingi pekee unaweza kosa kutosha kwa biashara ya siku moja yenye mafanikio.

Trader wa mwenendo wa bei, kwa mfano, anaweza kutumia utafiti wa kimsingi kutambua kampuni ambayo imetoa ripoti dhabiti ya mapato na kuna uwezekano wa kuona ongezeko la kiwango cha biashara na uwezekano wa bei kuwa juu kama matokeo. Kisha anaweza kufanya trade ya siku moja ya stock ya kampuni hiyo, akijaribu kufaidika kutokana na kuitikia kwa soko kwa ripoti chanya ya mapato.

Katika masoko ya crypto, traders wa mwenendo wa bei wanaweza kuunganisha maoni yao ya kiufundi na uchanganuzi wa kina wa sarafu ya msingi, habari, na simulizi zingine.

Kwa mfano, mnamo 2023, traders wamekuwa wakizingatia sana maendeleo ya kesi kati ya Ripple na Tume ya Usalama na Ubadilishaji ya Marekani. Maendeleo chanya ya kesi hii ya Ripple yalizua matokeo makubwa sana na kupata faida ya 100% kwa XRP kwa siku moja. Bila shaka, kuanzia sasa, traders wa crypto hujaribu sana kufuatilia matukio hayo.

Ingawa uchanganuzi wa kimsingi unaweza kutoa maarifa muhimu, traders wa siku moja wanapaswa pia kuzingatia mambo na mikakati mingine ya kupunguza hatari na uwezekano wa kuongeza faida.

Traders wa siku moja wanahitaji kuelewa kwamba katika trade ya siku moja kuna hatari kubwa za kifedha zinazohusika. Ili wasipoteze pesa, sharti traders wa siku moja watumie mikakati ya udhibiti wa hatari.

Orders za stop loss

Mkakati mmoja muhimu unahusisha kuweka order ya stop-loss, ambayo huonyesha kiwango cha hatari kilichoamuliwa awali ambacho trader yuko tayari kukubali kwa kila trade. Order ya stop-loss huchochea hatua ya uuzaji wakati bei ya stock inashuka kwa bei fulani, na kuzuia traders wa siku moja kupoteza pesa zaidi. Pia ni muhimu kwa traders wa siku moja kupunguza idadi ya stocks wanazonunua na kuuza kwa siku. Kuzingatia stocks chache zilizochaguliwa kwa trade ya siku moja inaweza kusaidia kupunguza hatari na kuongeza umakini.

Kugawa uwekezaji

Ingawa kugawa uwekezaji ni zana inayotumika sana kwa wawekezaji, traders wa siku moja wanaweza kuitumia pia. Kwa mfano, mkakati muhimu wa udhibiti wa hatari kwa traders wa siku moja ni kutoweka pesa zao zote kwenye trade ya siku moja. Vinginevyo, ni muhimu zaidi kuwa na angalau vipengee kadhaa kwenye taarifa za soko, za kuchagua kati ya zile zilizo na fursa bora za hatari/zawadi.

Dhibiti hisia

Kuruhusu hisia kudhibiti vitendo vyao vya biashara kunaweza kusababisha hasara kubwa kwa traders. Kujitahidi kupata faida kwa kila trade kunaweza kuwavuta traders wa siku moja katika kufanya ununuzi na uuzaji kutokana na tamaa, ambayo inaweza kuwafanya wapoteze pesa. Kwa hivyo, ni muhimu kwa trader wa siku moja kudumisha akili thabiti na mkakati wazi, unaowawezesha kufanya maamuzi ya ununuzi na uuzaji kuzuia hasara ambazo hazifai.

Ndio, unaweza kutumia trade ya siku moja kufanya trade ya safu. Safu ya kutrade, ambayo hutambuliwa kwa kutazama mitindo ya chati, hutumika kama zana ya msingi, kusaidia traders kutambua points za ununuzi na uuzaji. Mbinu hii hutumia dhana kwamba bei mara nyingi husonga kati ya viwango vya juu na vya chini ili kuunda safu.

Njia hii inaweza kutumika kwa crypto na mali nyingine, na kutoa fursa nyingi kwa traders wa siku moja. Hata hivyo, ni muhimu kukumbuka kuwa kuna hatari ya kifedha kwa mkakati wowote. Kwa hivyo, ni muhimu kwa traders kuelewa mifumo ya chati ndani ya safu ya biashara na kuunda mbinu za udhibiti wa hatari ili kupunguza hasara inayoweza kutokea.

Je, Ungependa kuanza biashara ya siku moja ya crypto?

Trade ya siku moja ya crypto inaweza kutoa fursa nyingi kwa traders wenye uzoefu na wanaoanza pia. Mikakati iliyojadiliwa, kama vile scalping na trade inayoendelea ya siku moja, hutoa njia tofauti za kuchunguza soko. Hata hivyo, ni muhimu kuelewa changamoto, kama vile kufanya biashara kupita kiasi, na haja ya kuchagua instruments na broker sahihi. Kufanya trade ya siku moja ya crypto ni mkakati dhabiti wa uwekezaji wa muda mfupi ambao unahitaji umakini wa mara kwa mara wa mabadiliko ya soko, lakini unaweza kutoa mapato makubwa kwa wale wanaoelewa mkakati huo. Kumbuka kila wakati, trader aliye na ufahamu mzuri hupata mafanikio.

Jinsi ya kuchagua broker sahihi

Wakati wa kuchagua trader anayefaa, ni vyema kuchagua aliye na leseni nyingi, uzoefu wa miaka kadhaa kwenye soko, ada zinazofaa na zenye uwazi, spreads na ada - na vipengele vingine vichache vyenye mafao. Kwa mfano, katika Exness tunatoa mafao ya kipekee, ambayo hayawezi kulinganishwa na brokers wengine, ambayo hutoa usalama kwa wateja wetu. Mafao haya ni pamoja na margin calls, seva za VPS kwa execution ya haraka na ya kutegemewa, uwekaji na utoaji fedha wa papo hapo, spreads za chini, na stop out na ulinzi dhidi ya salio hasi, pamoja na biashara ya swap-free katika maeneo fulani.

Ili kupata maelezo zaidi kuhusu ni akaunti gani ya kutrade inayokufaa, inafaa malengo yako, na mkakati wako, angalia aina mbalimbali za akaunti zetu.

Shiriki


Anza kutrade

Huu sio ushauri wa uwekezaji. Utendaji wa awali sio dalili ya matokeo yajayo. Mtaji wako uko hatarini, tafadhali fanya biashara kwa uangalifu.